
Bunge
la Taiwan, limeidhinisha mswaada wa kupiga marufuku uchinjaji wa paka
na mbwa, kwa matumizi ya binadamu.
Mswaada
huo pia umepiga marufuku wale wanaotumia gari au pikipiki kuwavuta
wanyama wao wa kuchezea, au kuwatanguliza wanaposafiri,na
atakayepatikana akienda kinyume, atakabiliwa na faini kubwa au
kufungwa hadi miaka miwili jela na majina na picha zao kuwekwa
hadharani.
Hatua
hiyo imeanzishwa ili kuboresha sheria za kuwalinda wanyama nchini
Taiwan, na ni moja ya aina yake kuanza kutekelezwa barani Asia.
Mwaka
2001, Taiwan ilipitisha sheria ya kupiga marufuku uuzaji wa nyama na
manyoya ya wanyama wa kuchezea kama vile paka na mbwa, kwa kile
kilichotajwa "madhumuni ya kiuchumi". Nyama ya mbwa, zamani
zilitumika kama chakula, lakini kwa sasa mnyama huyo anafaa
kujumuishwa kama mmojawepo wa wanafamilia.
No comments:
Post a Comment