Wasanii
hao waliowahi kutamba kitambo na wimbo Tunataabika, wamegeuka kuwa
madereva wa Bajaji.
“Tumekaa
kimya sana kwenye muziki kwasababu tulibadilisha fani baada ya kuona
kwenye muziki mambo yanatuvuruga tukaamua mimi hapa Dj Snox na
mwenzangu JB mkuu wa Majaji kuingia kwenye kazi mpya ya kuendesha
bajaji ili kujitafutia chochote kitu,” amesema Snox kwenye
mahojiano kipindi VMic cha Channel Ten.
“kazi
hio ndio tunaifanya mpaka leo hii na kituo chetu cha Bajaji kipo
Kariakoo Gerezani pale mwisho wa magari ya mwendokasi,” aliongeza.
Kwa
sasa Mabaga Fresh wana nyimbo mbili mpya, moja ni singeli inaitwa
MAISHA YA MTAA wamemshirikisha DOGO NIGA na wimbo mwingine unaitwa
KIDAWA ambao ndani yake wamemshirikisha Q-CHILLA,nyimbo
zote zimefanyika kwa producer D ambaye ndio kama meneja wao kwa sasa.
No comments:
Post a Comment