• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Monday, 10 April 2017

    Misri yatangaza miezi mitatu ya hali ya hatari.

    Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ametangaza miezi mitatu ya hali ya hatari nchini kote, kufuatia shambulizi la bomu ambalo limeua zaidi ya watu 40 katika makanisa mawili ya Coptic.

    Aidha Jeshi litapelekwa kusaidia polisi kulinda maeneo muhimu na vikosi vya usalama vitaruhusiwa kukamatwa bila kibali cha kukamatia,Kufuatia tukio hilo, Rais Abdel Fattah el-Sisi,ametangaza kuundwa kwa baraza litakalopambana na ugaidi na watu wenye itikadi kali.

    Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limekiri kuendesha mashambulizi hayo.

    Kundi la waislamu limejitokeza na kusesema kuwa kamwe shambulio hilo halitaweza kuwagawa Wamisri,Waislamu na Wakristo kwa pamoja wameungana nchini humo kupinga shambulizi hilo.

    No comments:

    Post a Comment