Timu ya Singida United baada ya kupanda ligi kuu imeendelea na jitihada za
kujiimarisha,kwa kuendelea kufanya usajili utakaoleta tija na
upinzani ligi kuu, baada ya kuwasajili wazimbambwe watatu Tafadzwa
Kutinyu kutoka Chicken Inn, Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa wote
kutoka Dynamos ya Zimbambwe sasa wako mbioni kufika Rwanda kwa ajili
ya kumsajili Danny Usengimana mshambuliaji hatari wa Polisi ya
Rwanda.
Habari
toka kwa mdau wa karibu zinaonesha kuwa Singida united wana nia ya
kupata saini ya mchezaji,mshambuliaji wa Amavubi ya Rwanda Danny
Usengimana, japo mpaka sasa Singida United hawajaweka wazi jambo hili.
Danny
Usengimana ni mchezaji hatari, katika msimu uliopita alitwaa tuzo ya
mchezaji bora wa ligi ya Rwanda.Na hii sio mara ya kwanza kwa wachezaji
kutoka Rwanda kuja kucheza Tanzania, Haruna Niyonzima ni miongoni mwa
wachezaji kutoka Rwanda anayecheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment