Nchini Nigeria watu saba walifariki dunia na wengine kujeruhiwa
baada ya kutokea hitilafu kwenye mfumo wa umeme walipokuwa
wakitazama mchezo kati ya Manchester United na Anderlecht.
Mashabiki hao wa soka waliokuwa wamekusanyika kwenye eneo
lililokuwa likitumika kuonesha mechi hiyo kupitia runinga huko kwenye
mji wa Calabar.katika mchezo huo “Manchester United” walishinda
2-1 kwenye mechi hiyo ya hatua ya robofainali ligi ndogo ya klabu
Ulaya, Europa League.
maafisa wa polisi walieleza kuwa, "watu 7 walikuwa wamefariki na wengine10 wamelazwa hospitalini na mmoja mmoja kati yao yupo chumba cha wagonjwa mahututi"
No comments:
Post a Comment