Ikiwa ni siku chache tu baada ya mastaa wa Bongo movie kulalamikia
wakitaka filamu za kigeni zizuiliwe nchini,watu malimabali wametoa
maoni yao juu ya jambo hilo na hata wengine kukosoa uamuzi huo.
Miongoni mwa watu waliotoa maoni yao juu ya ishu hii ya Bongo
movie ni Nikki wa pili toka Weusi,ambaye amefunguka kupitia Twitter
akaunti yake ametoa maoni yake kwa wasanii wa bongo movie kuwa
wanatakiwa wafahamike zaidi kwenye movie zao ili kulinda kazi zao
kama wafanyavyo wasanii wa nje.
“Movies za rambo ni maarufu kuliko rambo mwenyewe, bongo movies
tunawajuwa kwa vitu vingine zaidi wala hata sio movie zao.Ni kweli
tunahitaji kulinda soko la ndani, la movies lakini wao wanahitaji
kufanya tafakuri ya kina.
“Bongo movies mwanzoni walikuwa na soko, kuanza ni kujaribu, but
ku sustain is a science… mwendelezo wa lolote huitaji maarifa.Nchi
zote zilizoendelea zililinda masoko ya nyumbani, ndio tulilinde
lakini wenye movie nao wajilinde kwa kujiongeza kila kukicha.”
Ameandika “Nikki wa Pili”.
No comments:
Post a Comment