Wanamuziki
mbalimbali pamoja na wadau tofauti wa sanaa na muziki wamejitokeza
kwa wingi, katika mazishi ya baba wa staa wa muziki, Belle 9
aliyefariki akiwa hospitalini mkoa wa morogoro usiku wa Machi 18
akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na pikipiki.
Mzee
Damian amefariki dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa
kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa akiishi.,mzee huyo
wa mwanamuziki belle 9,alivunja mguu mmoja kwenye ajali hiyo na
baadae kuwahishwa hospitali,Dereva wa boda boda aliyemgonga nae
aliumia vibaya kupata majeraha kichwa.
Najua
kwa sasa Belle 9 yupo kwenye wakati mgumu kwa kumpoteza baba yake,
amabye amekuwa mwalimu wake kwa mengi katika maisha yake,Salamu za
pole kwa kijana wetu Belle 9 kwa msiba huu mzito na Mungu ailaze roho
ya baba yake mahali pema peponi.
No comments:
Post a Comment