Muungano wa vyama vya
upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) wamemteua Raila
Odinga kuwa mgombea kwa tiketi ya umoja huo kwenye uchaguzi mkuu
utakaofanyika Agosti mwaka 2017.
Bw Odinga sasa atakabiliana na Rais Uhuru Kenyatta
atakayetumia chama cha Jubilee kuwania muhula wa pili.“Hii ni
heshima kubwa sana ambayo ndugu zangu wamepatia, kwa kuniweka
nipeperushe bendera ya NASA.Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku
nyingi. Kila kitu tumeandika, tumekubaliana ya kwanza serikali
tutakayoiunda, ambayo ni serikali ya mseto itakuwa ni serikali ya
mpito,” ni maneno ya Odinga alpokuwa akihutubia baada ya kutangazwa
kuwa mgombea.
Alisema serikali yake itaangazia kumaliza umasikini,
kuimarisha afya, kuboresha uchumi, kubuni nafasi za kazi na kurejesha
gharama ya elimu na maisha chini,Aidha Odinga ameahidi kuhakikisha
walimu na madaktari,pamoja na wafanyakazi wengine wanalipwa mishahara
mizuri bila kusahau kutokomeza vitendo vya rushwa.
No comments:
Post a Comment