Naibu Waziri
wa mambo ya ndani ya nchini Tanzania Eng Hamad Masauni amesema kumekuwa na
matukio kadhaa ya Jeshi la Polisi, waandishi wa habari pamoja na
wananchi wa kawaida kufanyiwa fujo na baadhi ya watu hivyo serikali
itahakikisha inachukua hatua kali za kisheria kwa watuhumiwa.
Eng. Masauni
amesema”Uhalifu wa aina yoyote utakaofanywa na mtu au chama
chochote dhidi ya raia yeyote hatutokubali na tutachukua hatua kali
za kisheria”
“maeneo
yamkuranga,kibiti, na rufiji ni sehemu ambayo inaangaliwa kwa jicho
la tatu na tumejitokeza maeneo hayo kuwaomba wananchi wasaidiane na
jeshi la polisi kwa kujenga mahusiano mazuri ili kusaidiana kupata
taarifa za wahalifu”
“Serikali
inajipanga kufikisha huduma za upatikanaji wa leseni na
miundombinu,kwa wananchi wa eneo la Tarime Rorya,aidha tunatarajia
kufikisha huduma kwenye mikoa yote mipya na maeneo ambayo huduma za
utoaji leseni,na kujenga miundombinu kulingana na bajeti yetu.”
Alimaliza
kwa kusema ili sheria isiweze kukukumba,ni vyema ukaishi kwa kufuata
sheria na kanuni na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment