Real
Madrid yaitikisa LaLiga baada ya kuitwanga Derpotivo la Coruna kwa
mabao 6-2,ingawaje nyota wake kadhaa kutokuwepo dimbani, kama
Cristiano Ronaldo(CR7),Karim Benzema, lakini kikosi cha Madrid
kilioneka kuwa bora kuwazidi wapinzani wao Derpotivo ambao walikubali
kibano kikali ambacho hata hivyo kinawafanya wawe nyuma ya Barcelona
baada ya kuzidiwa magoli wa kufungwa na kushinda.
Madrid
ilipata mabao yake kwa kupitia wachezaji wake,James Rodrigues mabao
mawili huku, Casemiro,Lucas Vazquez, Isco na Alvaro Morata kila
mmoja akifunga goli moja na kuipa timu yao ushindi huo.
Derpotivo
ilipata mabao mawili kupitia Florin Andone na Joselu ambayo
hayakuwasaidia kubadili matokeo ya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment