“Salaam dada angu
@rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit
ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa
wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….
Nafarijika kuona
wimbo wako wa #Unanimaliza' watu mbalimbali wameupokea vizuri,na
nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu
wako mpya….
Ombi langu kwako
usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto
nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu
na kumuomba Muumba, itapita….
Niwaombe pia Vyombo
vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa
sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake
kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu
ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….
InshaAllah Mwenyez
Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila
siku@rayctanzania” Chibu alimalizia kwa kuandika haya kupitia ukurasa wake wa instagram
No comments:
Post a Comment