Kwenye Ligi Kuu
yaUbelgiji KRC Genk inayochezewa na mchezaji machachari mtanzania
“Mbwana Samatta” walikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa 5 wa play
off wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya wenyeji wao AS Eupen.
KRC Genk
wakiwa na rekodi nzuri ya kuwa timu pekee katika timu 12 zinazocheza
game za play off kutofungwa katika mchezo hata mmoja wakiwa
wameshinda michezo minne,ambapo april 26 /2017, KRC Genk wamejikuta
wakilazimishwa sare ya kufungana kwa goli mojamoja(1-1) walipokuwa
ugenini na kuwafanya kupata sare ya kwanza.
AS Eupen licha
ya kuwa nyumbani walifungwa goli la mapema kwenye dakika ya 20 ya
mchezo,bao lililopachikwa na”Malinovsky” akipachika goli la
kwanza la Genk lakini AS Eupen walisawazisha goli hilo dakika ya 51,
katika michezo ya play off KRC Genk na AS Eupen ndio timu pekee
ambazo hazijapoteza mchezo katika timu 12 kwenye kundi A na B.
No comments:
Post a Comment