Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametoa tahadhari kwa mtu
yeyote yule atakayejaribu kuvunja muungano uliopo kati ya Tanganyika
na Zanzibar, na kwa kushirikiana na mwenzake ambaye ni Rais wa
Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein
Kwa msisitizo ameomba
wananchi wote kujua umuhimu na kuwa na moyo wa kuuenzi na kuulinda
muungano wa nchi hizo mbili zinazokamilisha jamhuri ya muungano wa
tanzania,ambapo onyo hilo amelitoa leo mjini Dodoma wakati wa
maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
yaliyofanyika mjini Dodoma.
Lakini pia Rais
Magufuli(JPM) amekiri kuwa anatambua kuwa licha ya mafanikio
yaliyopatikana kwenye muungano huu, pia bado kuna changamoto
mbalimbali zinazoukabili Muungano,hivyo kuulinda muungano kwa kutatua changamoto za muungano ni suala ambalo kwenye awamu yake litazingatiwa ili kuimarisha muungano na kutimiza ahadi alizozitoa kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment