• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Saturday, 8 April 2017

    Timu ya Yanga kifua mbele Taifa leo dhidi MC Aalger ya Algeria

    Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, Yanga SC wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya MC Aalger mchezo uliochezwa leo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
    Goli hilo la Yanga limefungwa na kiungo "Thabani Kamusoko" dakika ya 61 alipopewa pasi na Chirwa karibu na eneo 18 upande wa goli la MC Alger, Kamusoko hakufanya ajizi na kuitumia nafasi aliyoipata kuwapa burudani mashabiki.
    Mshambuliaji Donald Ngoma aliongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga akisaidiana na Obrey Chirwa ambaye alikuwa kwenye kiwango kizuri kwenye mchezo wa leo licha ya kukosa nafasi kadhaa.



    Japo wageni wa Yanga waliendelea kutumia mbinu za kimpira za ukanda wa Kaskazini mwa Afrika,kwa wachezaji wa MC Alger kujiangusha angusha na kupoteza muda lakini bado mambo yaliwawia ngumu na mchezo kumalizika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa goli 1-0.

    No comments:

    Post a Comment