Taarifa
iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii na kushika hatamu kwenye
vyombo vingi vya habari juu ya kutoweka kwa msanii roma mkatoliki na wenzake,imepata ufumbuzi baada ya kupatikana jana,mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.
J
Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na
wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, ameeleza kuwa
wasanii hao wamepatikana.
Lakini
pia Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga
amethibitisha kupatikana kwa wasanii hao,na walipitia kituo cha
polisi Oysterbay kwa mahojiano nao ya kipolisi.
Baabda ya kutoka kituo cha polisi Oysterbay Roma kwa niaba ya wenzake,alizungumza kwa kifupi na kusisisitiza;
"Sisi wote ni wazima kabisa kimwili na kiakili,na tuwashukuru watanzania wote kwa ujumla na vyombo vya habari vyote,tutazungumzia kile kilichotokea jumatatu kwenye media panapo majaaliwa tunaomba tukapumzike kwa sasa".
No comments:
Post a Comment