Jeshi
la Marekani limezielekeza meli zake za kivita zielekee karibu na rasi
ya Korea,meli hizo zikiwa zimebeba silaha za kivita ni baada ya korea
kaskazini Kufanya majaribio ya silaha zake kwa kuimarisha silaha zake
za kinyukilia.
Msimamizi
wa kijeshi wa Marekani ukanda wa Pacific ameeleza kuwa kujiandaa huko
kijeshi ni muhimu sana, Meli hizo zinajulikana kama ”The Carl
Vinson Strike Group” zina meli moja kubwa ya kubeba ndege za kivita
na meli nyingine za kawaida za kivita zikiambatana nayo.
Msemaji
wa jeshi la Marekani anaitazamia Korea Kaskazini kama tishio kubwa
zaidi kwa usalama wa eneo la Pacific.
Anasema
ushahidi ni jinsi taifa hilo linavyofanya mazoezi ya zana za
kinukilia kiholela.Meli hizo maalumu zinauwezo mkubwa katika kufanya
mashambulizi na kujizuia na makombora ya maadui.
No comments:
Post a Comment