Diamond platnumz ameandika haya kupitia ukurasa wake wa instagram;
"diamondplatnum Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟..... lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa... Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: "mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea....ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea..."
Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza...nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana...ikapelekea hadi kufikia hapa...asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭
Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua mzee wa single touch ukimuamulia mtu....... naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁😆😅"
Hii imetokea baada ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la "Acha nikae kimya" kumtaja "Askofu Gwajima" kwenye mashairi yake,ambapo Diamond ameeleza mambo mbalimbali yaliyotokea nchini likiwemo la msanii Roma mkatoliki kupotea katika mazingira ya kutatanisha kabla ya kupatikana juzi
#Acha nikae kimya
No comments:
Post a Comment