Mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho (FA) Yanga, wametinga hatua ya nusu
fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
dhidi ya Tanzania Prisons,ambapo mchezo ambao umefanyika katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,kwa sasa yanga inaungana na timu
za Simba, Azam na Mbao FC katika hatua ya nusu fainali ambapo droo
inasubiriwa.
Tanzania
Prisons kwenye mchezo wa leo walipata penalti dakika ya 54 lakini
mpigaji Victor Hangaya aligongesha mwamba,Baada ya ushindi huo, Yanga
inakamilisha timu nne za nusu fainali, droo ya hatua hiyo itafanyika
siku ya kesho tarehe 23 april,2017 ili kuzitambua timu zitakazokutana
nusu fainali.
No comments:
Post a Comment