Jeshi
la Kenya limesema kuwa limewaua wapiganaji zaidi ya 50 wa Al-Shaabab
katika oparesheni maalumu iliyofanywa Kusini mwa Somalia.
Jeshi
hilo limedai kuwa walinasa shehena ya silaha na risasi na kuharibu
kabisa kambi ya wapiganaji hao katika eneo la Badhaadhe katika Lower
Juba,hadi wakati huu Al Shaabab hawajasema lolote.
Maelfu ya wanajeshi wa Kenya wanahudumia nchini Somalia chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika,imekuwa mara kadhaa kwa kundi la kigaidi la Al Shaabab hufanya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye mpaka na Kenya na pia kwenye kambi za wanajeshi wa Kenya walioko Somalia.
No comments:
Post a Comment