Ni wiki kadhaa zimepita tangu “Roma Mkatoliki” na wenzake watatu, Moni, Imma
na Bin Laden, walipotekwa wakiwa kwenye Studio ya Tongwe Records
iliyopo Masaki, habari zilizopo kwa sasa kwamba studio hiyo imefungwa
na haifanyi kazi kwa sasa.
J Murder wa tongwe records amedai studio hiyo itafunguliwa mara tu baada ya mambo kukaa sawa.
“Ni kweli Studio kwa sasa haifanyi kazi kwa sababu watu bado hawajakaa sawa, wanahitaji kupunzika kwanza,” alisema Murder. “Mimi nadhani kwa sasa afya ya vijana wetu ndio kipaumbele cha kwanza, mambo yakitulia kila kitu kitakuwa wazi,”
Tumeamua
kupumzika kwa muda wakati vijana wakituliza akili ili kila mmoja
aweze kurudi katika hali yake ya kawaida na kwa waliopata majeraha
waweze kupona kabisa,pia ni muda ambao wenzetu jeshi la polisi
wanaendelea na uchunguzi wa tukio zima.
No comments:
Post a Comment