Mwaka
2017 na kumiminika kwa watalii Tanzania ambapo mastaa na watu
mashuhuri wameweza kuzulu kwa lengo la kutalii nchini,ambapo watu
kama mwigizaji maarufu wa filamu kutokea Hollywood nchini
Marekani,”Will Smith na mkewe Jada Pinkett-Smith” pia
mwanamitindo na mrembo, Chanel Iman,aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa
Taifa la Israel, Bw. Ehud Barak,kwa nyakati tofauti waliweza
kutembelea mbuga ya wanyama ya serengeti na vivutio vingine kama
hifadhi ya taifa ya ngorongoro.
Ngorongoro
huendwa zaidi kwakuwa ina historia kubwa sana na watu tofauti hupenda
kuifuatilia historia hiyo na kutazama mandhari ya kuvutia,lakini pia
kwakuwa ndani ya hifadhi hii kabila la wamasai limejikita humo na
kuendeleza maisha pasipo kuleta athari kwa wanyama pori waliomo humo.
Masalia
ya Kale ya Binadamu wa Mwanzo. Ngorongoro ndimo linapopatikana bonde
la Olduvai ambalo kwa mujibu wa wanahistoria yanapatikana masalia ya
binadamu wa mwanzo kuishi duniani. Hapa ndipo wanaikolojia maarufu
Dkt. Louis na mkewe Mary Leakey walipata masalia ya kale likiwemo
fuvu la mtu wa kale zaidi, Zinjanthropus, ambaye alipata kuishi miaka
milioni 1.75 iliyopita. Utafiti wao uliweza kuvumbua mabadiliko ya
taratibu ya ukubwa wa ubongo na zana zao za mawe walizokuwa
wanazitumia.
Maziwa
kama Ziwa Ndutu na Masek,mlima Oldonyo Lengai ulio nje kidogo ya
hifadhi amabo una uasili wa kuwa na volkeno,pia kuna ndege wa aina
tofauti kama flamingo ambao wanazidi kuleta mvuto wa pekee.
Mtu
yeyote kutoka pande yoyote ya dunia hii anaweza kufanya utalii na
kujionea ,vivutio vingi vipatikanavyo ndani ya hifadhi hii ya
ngorongoro,lakini pia kuna sehemu nyingi sana ambazo utajionea mengi
ya kustaaajabisha na kukuvutia,mimi na wewe tunaweza kufika kwenye
maeneo haya na tukawa mabalozi wazuri kwa wengine kwenye maeneo
tutokayo.
No comments:
Post a Comment