Mbunge
wa viti maalum CCM katika mkoa wa Songwe “Juliana Shonza” amesema
anawashangaa baadhi ya wabunge ambao mara kwa mara wamekuwa
wakisimama bungeni na kwenye majukwaa wakisema kuwa serikali
haijafanya kitu kwa ajili ya wananchi wake.
Haya
ameyasema alipokuwa bungeni na alipokuwa anachangia juu ya bajeti ya
Tamisemi,akisema baada ya kutolewa kwa elimu bure,idadi ya udahili wa
wanafunzi kwa elimu za shule ya msingi umeongezeka na hata pia
wanafunzi waliokuwa wanarubuniwa kwa sasa mambo yamebadilika.
Amesisitiza
kwa kusema ,kikubwa ni ushirikiano baina ya viongozi wote
wanaowatumikia wananchi,walimu wapewe motisha ili kuweza kufanya kazi
kwa moyo na kwa uzalendo kabisa,ameiomba serikali isiishie kuwapa
motisha walimu wakuu pekee bali kuwawezesha walimu wote kwa kuwapa
motisha itakayowapa nguvu na moyo zaidi katika uendaji kazi na
kulitumikia taifa.
No comments:
Post a Comment