SIMBA
SC wameshindwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
baada ya kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji Kagera Sugar Uwanja wa
Kaitaba, Bukoba jioni ya leo.
Ushindi
huo unaifanya Simba SC ibaki na pointi zake 55 baada ya kucheza mechi
25 na kuwaacha, mabingwa watetezi Yanga SC wakiendelea kuongoza Ligi
Kuu kwa pointi moja zaidi na Kagera Sugar inaendelea kukaa nafasi ya
tatu kwa pointi zake za mechi 25.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa Jimmy Fanuel, aliyesaidiwa na Joseph Masija
wa Mwanza na
Geoffrey
Msakila wa Geita,hadi mapumziko Kagera Sugar walikuwa mbele kwa bao
1-0.
Bao
hilo lilifungwa na mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania,
Mbaraka Yussuf Abeid dakika ya 27 kwa shuti kali la umbali wa mita 22
baada ya pasi ya mchezaji mwenzake wa zamani wan Simba B, Edward
Christopher.
Simba
wakaamua kufunguka baada ya bao hilo na kuanza kupeleka mashambulizi
ya moja kwa moja langoni mwa Kagera Sugar.
Na
Laudit Mavugo, Said Ndemla na Abdi Banda wote wakapoteza nafasi nzuri
za kufunga wakiwa wamebaki na kipa Juma Kaseja.
Nafasi
ambayo wataijutia zaidi Simba SC ni ya beki Banda dakika ya 43 ambaye
alifanikiwa kuipata pasi nzuri ya beki wa kushoto Mohammed Hussein
‘Tshabalala’ na kuwatoka mabeki wawili wa Kagera Sugar, lakini
shuti lake dhaifu likadakwa na Kaseja aliyekuwa hatua mbili tu kutoka
kwake.
Kipindi
cha pili, kila timu ilifanikiwa kupata bao moja, Kagera Sugar
wakianza kupitia kwa Edward Christopher aliyemalizia pasi ya Sulemani
Mangoma dakika ya 47 kabla ya Muzamil Yassin kuifungia Simba bao la
kufutia machozi dakika ya 67 akimalizia pasi ya Mghana, James Kotei.
Baada
ya hapo, timu hizo zikaanza kushambuliana kwa zamu na sifa zimuendee
kipa mzoefu, Juma Kaseja aliyeokoa michomo kadhaa ya hatari ya Simba.
Kikosi
cha Kagera Sugar kilikuwa; Juma Kaseja, Godfrey Taita, Mwaita Gereza,
Juma Shemvuni, Mohamed Fakhi, George Kavila, Suleiman Mangoma, Ame
Ally ‘Zungu’/Ally Ramadhani, Edward Christopher/Themi Felix,
Mbaraka Yusuph na Japhet Makalai/Anthony Matogolo.
kIkosi cha Simba SC leo kilikuwa hivi; Daniel Agrey, Muzamil Yassin, Mohammed
Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Juuko Murshid, Jonas Mkude,
Shiza Kichuya/Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla/Juma Luizio, Laudit Mavuo,
Ibrahim Hajib/Mohammed Ibrahim na James Kotei.
No comments:
Post a Comment