Mwanamuziki huyo aliyejaliwa sauti yenye mvuto amedai
kuwa baada ya Diamond na Belle 9 kuachia nyimbo zao walizotumia
baadhi ya vionjo vya kwenye wimbo wake wa ‘Maria Salome’ ndipo
akapata nguvu mpya ya kurudi muziki na kudhamiria kuimarisha kile
kilichomo ndani yake.
Pia mwanamuziki huyo alidai kuwa lishaanza safari ya
kwenda kuanza maisha mapya kijijini kwao.
“Nilishatamani kuacha muziki na nilishawahi
kuhamisha baadhi ya vitu vyangu kurudi kijijini na ndiyo kipindi
hicho hicho ambapo Diamond na Belle 9 walitoa nyimbo ya salome, na
hatimaye wakanirudisha maana ilikuwa safari kabisa,” amekiambia
kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii.
No comments:
Post a Comment