
Chanjo
ya kwanza ya malaria duniani itajaribiwa kusambazwa mwaka ujao na
imewekwa kipaumbele katika nchi kama Ghana, Kenya na Malawi kuanzia
mwaka ujao,WHO limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu
ya watu,ambapo mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi
ya watoto laki saba wenye umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na
nusu.
Tafiti
mbalimbali zimeshafanywa juu ya kuweza kumaliza tatizo la ugonjwa
huu,na zinaonekana kuzaa matunda kila uchwao,chanjo hiyo
inayotarajiwa,itaenda sambamba na mbinu mbadala zinazoendelea
kutumika kwa kujikinga na malariakama vile neti, dawa za kufukuza
mbu, na dawa za kukinga malaria.
No comments:
Post a Comment