Klabu ya soka ya Newcastle
united imefanikiwa kupanda daraja na kurudi katika ligi kuu baada ya
mwaka jana kushuka dimbani ikiwa chini ya kocha Rafa Benitez.
Newcastle imefanikiwa kupanda
daraja baada ya kuibamiza mabao 4-1 timu ya Preston North End inayo
shika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi daraja la kwanza
(championship),Newcastle chini ya kocha Benitez imeshika nafasi ya
pili kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza ikiwa chini ya Brighton
ambayo nayo imepanda daraja.
Katika mchezo huo dhidi ya
preston,magoli ya Newcastle yalifungwa na Ayoze perez mawili huku
mchezaji raia wa Ghana Christian Atsu akifunga moja na Matt Ritchie
akifunga moja kwa mkwaju wa penati,Matokeo hayo ndio yameifanya
Newcastle kurudi ligi kuu na mwakani tutashuhudia michezo mbalimbali
katika uwanja wa nyumbani wa Newcastle St James Park
No comments:
Post a Comment