Baada ya shirikisho la soka
Tanzania TFF kumaliza mzozo cha mzozo wa point 3 zilizokuwa
zinawaniwa na Simba na Kagera Sugar,baada ya Simba kufungwa April 2
kwa magoli 2-1 na baadae kukata rufaa kwa madai ya Kagera kumtumia
mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano kinyume na
taratibu.
Ambapo kamati ya katiba na hadhi za
wachezaji iliwarudishia kagera sugar pointi zao na magoli kama
yalivyokuwa mwanzo,na kuhitimisha juu ya mzozo huo.na hapo ndipo
wadau tofauti wa soka walipokuja na ushauri tofauti kwa chama cha
mpira wa miguu Tanzania.
Mmoja wa watu waliotoa ushauri ni
Katibu Mkuu wa Yanga “Charles Boniface Mkwasa” ambapo leo ametoa
ushauri kwa shirikisho la soka Tanzania TFF kuhusiana na kanuni
iliyopo ya timu ambayo inamchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu
za njano kunyan’ganywa point 3 na kupewa mpinzani wake, Mkwasa
ametoa ushauri kuhusu kipengele hicho.
No comments:
Post a Comment