Rais
wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi,ampost kwenye
mitandao ya kijamii na kusema. “hongereni wana mwanza kwani Uwanja
wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumiwa kwa mechi za
Kimataifa,” ametweet Malinzi.
Hii imekuja baada ya wataalamu wa Ufundi wa CAF kuzulu Mwanza na kuukagua uwanja huo mwishoni mwa mwaka jana.
Viwanja
vingine ambavyo vinatambulika na CAF pamoja FIFA kwa kutumika na
michezo ya kimataifa ni pamoja “Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam
Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam”.
Kupitishwa
kwa CCM Kirumba kuna ongeza wigo wa kuwa na viwanja vingi
vitakavyotumiwa na michezo ya mechi kubwa za kimataifa kama zile za
fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa
za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Viwanja
vingine ambavyo vimekaguliwa na na vinasubiri majibu ya kupitishwa
kwake ni Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya na Kaitaba wa Kagera.
No comments:
Post a Comment