Harmonize
ambaye ni msanii mkubwa ndani na nje ya Tanzania ,pia ndiye msanii wa
kwanza kusainiwa na lebo ya muziki ya WCB,na amekuwa akiendelea
kudondosha ngoma kali kila anapofanya ngoma zake,amesema siri pekee
ya yeye kuendelea kufanya nyimbo nzuri na zenye ubora ni kutokana na
kufuata nyayo za bosi wake “Diamond platnumz” ambaye amekuwa
akifaya kazi kwa bidii kila wakati,ijapokuwa ndiye msanii mwenye
mafanikio makubwa Tanzania.
Aidha
Harmonize anayemiliki tuzo ya Afrimma amezulu(+254) Kenya na kama
ilivyo ada, "Mzazi Willy" Tuva alimkalisha Msetoni na kupiga naye story
kadhaa,na alisisitiza kwa kusema tunavyoongea Diamond yupo South
Africa kwa ajili ya kazi”
Aliongeza
kwa kusema“Kama Diamond ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa
Tanzania na hana time ya kujiachia,hiyo inanipa nguvu kuzidi kupambana
na mimi,” na alihitimisha kwa kuwaomba mashabiki wa muziki wake
kukaa macho kwenye mtandao wa wasafi.com kwani muda wowote kuna kitu
kizuri kinakuja
No comments:
Post a Comment