Rais
John Pombe Magufuli wa Tanzania amepokea kwa mshtuko mauaji ya askari
polisi nane waliouawa na watu wasiojulikana jioni siku ya tarehe
13/04/2017.
Taarifa
kwa vyombo vya habari na vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa askari hao
walitoka kwenye mpango kazi wao wa kawaida,ndipo waliposhambuliwa na
watu wasiojulikana kwa kupigwa risisa kwenye eneo la mpakani mwa
wilaya ya Kibiti mkoani Pwani,ambapo walikuwa na usafiri wa gari.
Rais
Magufuli amelaani tendo hilo na matukio yote ya kuwashambulia polisi
akisema wanafanya kazi kubwa ya kuwalinda raia,ametuma salamu
za rambirambi kwa jamaa na marafiki walioguswa na vifo hivyo huku
akiwataka raia wote kushirikiana katika kukomesha vitendo kama hivyo.
''Nimeshtushwa
na kusikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao wamepoteza
maisha wakiwa wanalitumikia taifa, naungana na familia za marehemu
wote, jeshi la polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu
cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu,namuomba
mungu atupe moyo wa subira ,uvumilivu na ustahimilivu'',alisema
rais Magufuli
No comments:
Post a Comment