Mradi
wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
pamoja na mradi wa nyumba za wananchi Magomeni pale Magomeni
Kota,utazinduliwa jumamosi hii.
Miradi
hiyo miwili itazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli jumamosi hii,ambapo mradi wa hosteli hizo
unakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 10 zitakuwa na uwezo wa kumudu
zaidi ya wanafunzi 3,840.
Hizi
zitakuwa hosteli za wananchi wa chini kabisa kama ambavyo Rais wetu
amekuwa akieleza nia yake ya kuwasaidia wananchi wa chini,na mpango
ni kufanya kila mwanachuo atakayekuwa akitumia hosteli hizo awe
akilipa shilingi laki moja na elfu kumi tu kwa muhula mzima,ambacho
ni kiwango cha chini ukulinganisha na kodi za hosteli zilizopo
mitaani.
Aidha
kesho mara baada ya Uzunduzi huo, Rais Magufuli pia anatarajiwa
kuweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa nyumba za Magomeni kota.
No comments:
Post a Comment