
Kwenye
kipindi cha “The Weekend Chart Show” jana 14 april 2017
kinachorushwa na Clouds TV msanii rapa Bill Nass ambaye anatamba na
na ngoma kali inayokwenda kwa jina la” Mazoea” amemsihi Roma
Mkatoliki na wenzie ambao walikumbwa na mkasa wa kutekwa.
Bill
Nass amewataka Roma na wenzie kuendelea na maisha kwa kufanya kazi
ingawa hawatokuwa vizuri lakini kwa sababu wana uhai na ni wazima
hicho pekee katika maisha yao wanapaswa kumshukuru Mungu.
"Wanapaswa
kumshukuru Mungu kwa kuwa wameendelea kuwa hai,hivyo waendelee
kufanya kazi kwa moyo ule ule, natambua inakuwa ngumu kiasi hasa
unapokuwa na kumbukumbu mbaya kichwani ile pressure haikupi mzuka wa
kufanya kazi.Kwa mfano, mimi tu nikiwa hivyo mood za studio zinakata.
Japo wao wanaweza kuwa zaidi ya hapo,kiujumla hizo ni changamoto,so,
isiwafanye wakaishia hapo as long as wako hai na wazima."Bill
Nass.
No comments:
Post a Comment