Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli amezindua
hostel mpya za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa hosteli hizo zenye uwezo wa kuchukua
takribani wanachuo 3,840.
Hii
imekuja baada ya Rais Magufuli kufanya ukaguzi wa hosteli hizo mwezi
Septemba,mwaka jana 2016,wakati ujenzi wake ulipokuwa ukiendelea,na
wakala wa Majengo nchini TBA ndio waliosimamia zoezi zima mpaka
ujenzi huo kukamilika.
Hii
italeta nafuu na fursa ya vijana na wananchi wa kitanzania kupata
huduma hiyo kwa gharama za chini kabisa,mungu ibariki Tanzania na
viongozi wetu wote.
No comments:
Post a Comment