Maafisa wa
usalama wa Afghanistan wanasema zaidi ya wapiganaji 90 wa kundi la
kigaidi la Islamic State(IS) waliuawa na bomu kubwa lililodondoshwa
na Marekani alhamisi hii.
Hapo awali idadi
iliyokisiwa inaweza kuwa ni mara mbili ya idadI ya sasa,lakini Islamic State
wamekanusha taarifa hizo kwa kusema hawampoteza mtu yeyote kwenye tukio la kombora hilo.
Kamanda wa
kijeshi wa Marekani nchini Afghanistan, Jemedari "John Nicholson",alisema kuwa Marekani iliamua kutumia bomu kubwa zaidi katika
mashambulizi hayo kutokana na mbinu kabambe za kijeshi dhidi ya
magaidi.
No comments:
Post a Comment