Michezo ya
robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mechi zilizochezwa
jana april 18/04/2017, kwenye mechi za marudiano klabu mbili za jiji
moja la “Madrid” huko hispania ziliweza kufuzu kuingia hatua ya
nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, inayojulikana sana
kama;“UEFA Champions League”.
"Atletico Madrid" ambayo ilipewa
baraka za kuingia kwenye hatua ya nusu fainali na "Leicester City" ya
Uingereza baada ya kumaliza mchezo wao kwa sare ya mojamoja(1-1), na
kwakuwa Atletico ilipata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa
kwanza,hivyo sare yao ya jaja imeiwezesha Atletico kufuzu hatua
inayofuata.

Ambapo "Real Madrid" kwa upande wao ndani ya dk 90 za kawaida,walitanguliwa na "Bayern Munich" kwa goli 2-1,na baada ya kupewa muda wa ziada ndipo madrid walipofanya maajabu kwa kupiga goli tatu ndani ya dk 30 za nyongeza,ni hapo CR7 alipokamilisha Hat Trick na goli moja likifungwa na Marco Asensio,na mpaka kipenga cha kuhitimisha mchezo huo ubao ulisoma 4-2.
No comments:
Post a Comment