Mbunge wa Mikumi mh "Joseph Leonard Haule" maarufu kama Professor J, leo April 19, 2017 alisimama Bungeni kuuliza maswali kwa serikali juu ya changamoto ya maji zilizopo jimboni kwake na majibu yakatolewa na Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Isack Kamwelwe.
Aidha
serikali imemuahidi mbunge na wananchi wa jimbo la mikumi mradi wa
maji millioni 809.4 kukamilika ifikapo mwezi mei mwaka huu,mradi
utakuwa umekamilika kwani kwa sasa mradi umekamilika kwa asilimia
80,na pia serikali amewaahidi kufanyia marekebisho ya vyanzo vingine
vya maji,kama “madibila na segereti”,na kwakuwa naibu waziri
amekiri kuwa alikwisha tembelea maeneo hayo ya jimbo la mikumi wana
mikumi wasubiri kumalizwa kwa kero hiyo miezi michache ijayo.
No comments:
Post a Comment