Mwizi
wa simu alikamatwa kwa kutumia programu ijulikanayo kama “Find My
iPhone” na hatimae zilipatikana simu alizoiba,Simu hizo zilikuwa
zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo la
California, polisi wameripoti.
programu(App)
hiyo huonesha ilipo simu,hivyo baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu
zao kutoa taarifa kwa polisi, maafisa wa polisi walifuatilia kwa
kutumia app hiyo hadi wakafanikiwa kumnasa mshukiwa wa tukio hilo la
wizi.
Maafisa
Walimkuta mshukiwa huyo na simu zaidi ya simu 100 zikiwa kwenye mfuko
wake,ambapo baadae simu zilirudishwa kwa wenye nazo,na nyingine
kuhifadhiwa mpaka wenyewe wakipatikana.
No comments:
Post a Comment