• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Thursday, 20 April 2017

    Juventus na Monaco nazo zafuzu hatua ya nusu fainali UEFA champion league.

    Monaco wamemaliza mchezo wao dhidi yaBorussia Dortmund na ushindi wa bao 2 -1,mabao yaliyofungwa na Kylian Mbappe na Falcao kwa upande wa Monaco na bao pekee la Dotmund likiwekwa kambani na Marco Reus.

    Uwanja wa nyumbani wa Barcelona Nou Camp,mambo yamekuwa magumu kwa wenyeji Barcelona kuondolewa katika michuano ya UEFA baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana.

    Ambapo Katika mchezo wa kwanza Barcelona ilichakazwa bao 3, walipokuwa ugenini hivyo matokeo ya sare yamewafanya kuondolewa katika michuano hiyo.Matokeo hayo ni chanya kwa upande wa Juventus na Monaco inawafanya kufuzu katika hatua ya nusu fainali wakitanguliwa na Real Madrid na Atletico Madrid.

    No comments:

    Post a Comment