Kundi
la Al-Shabab latoa onyo kwa wazazi nchini Somalia, kwamba
wasiwapeleke watoto wao katika shule na vyuo vikuu visivyokuwa vya
Kiislamu.
Kundi
hilo limedai kwamba mfumo wa elimu wa magharibi unazorotesha
maadili,msemaji wa kundi hilo “Ali Mohamoud Rage” ameonekana
kwenye mkanda wa video, akisema mtu yeyote akijihusisha na elimu
inayoeaneza mila na tamaduni za kigeni watakabiliana nae vilivyo.
Hivi
karibuni al-Shabab lilizindua mtaala wake wa elimu kwa lugha ya
kiarabu,na kwa upande wa serikali ya Somali imelishutumu kundi hilo
kwa kujaribu kuwanyima watoto wa Kisomali elimu bora huku wakiendelea
kupandikiza itikadi yao inayosimamia mapigano na mauaji.
No comments:
Post a Comment