Hayo yamesemwa na makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kufanya
ziara katika bwawa la Kuzalisha umeme la Mtera ili kuona utendaji
kazi kwenye Bwawa hilo baada ya kumaliza ziara mkoani Iringa.
Makamu
wa Rais amesema uharibifu mkubwa unaondelea kwenye mito
inayotiririsha maji kuelekea bwawa la Mtera ndio chanzo cha maji
kuendelea kupungua mwaka hadi mwaka hivyo hatua za kukabiliana na
hali hilo ni lazima zikuchuliwe ili kukokoa bwawa hilo kukauka.
Amesisitiza
kuwa kutokana umuhimu wa bwawa hili la Mtera,linalotuletea umeme
mkubwa nchini ni muhimu wafanyakazi,wa bwawa hili wawe wazalendo na
ili liendelee kuleta tija kwa nchi nzima kwa maendeleo ya viwanda na
shughuli za uzalishaji kwa ujumla.
Meneja
wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera Mhandisi “John Sikauki' alitoa
taarifa ya hali ya uzalishaji Umeme kwenye kituo hicho kwa makamu wa
Rais, amemueleza Makamu wa Rais kuwa hali ya mitambo ni nzuri ambapo
mpango wa matengenezo katika kituo hicho Umefanyika.
Meneja
wa kituo alimuomba makamu wa rais mama Samia Suluhu,kuwa serikali
iweke mkazo kwenye uhifadhi wa bonde la mto ruaha ambalo ni moja ya
chanzo kikuu cha maji yanayonufaisha uzalishaji wa umeme.
No comments:
Post a Comment