KRC Genk anayoichezea mtanzania “Mbwana Samatta” usiku wa 13/04/ 2017 waliingia uwanjani kucheza mechi ya Europa League dhidi ya Celta Vigo kwenye uwanja wa Balaidos Hispania.
Mchezo huo ulikuwa ni robo fainali ya kwanza ,ambapo KRC Genk walikuwa ugenini,mpaka mchezo unamalizika Genk walijikuta wakiambulia goli 3-2.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na “Jean Boetius dakika” ya 10 na “Thomas Buffel” aliyeingia akitokea benchi dakika ya 68, kwa upande wa Celta vigo magoli yao yalifungwa na “Pione Sisto” dakika ya 15, “Iago Aspas” dakika ya 17 na “John Guidetti” dakika ya 38, kwa matokeo haya Genk katika mchezo wa marudiano Luminus Arena April 20 watalazimika wapate ushindi wa kuanzia goli 1 na zaidi ili wafuzu nusu fainali.
“Mbwana Samatta” ambaye amekuwa na rekodi nzuri amecheza mechi hiyo kwa dakika zote 90 lakini hakufanikiwa kupata goli mpaka kipenga kilipohitimisha mchezo huo.
No comments:
Post a Comment