• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Friday, 14 April 2017

    Kamati ya saa 72 imeipa simba pointi 3,na magoli matatu kwenye rufaa dhidi ya Kagera sugar

    Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 imeipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu kutokana na rufaa waliyoikatia Kagera Sugar kwa kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 2, mwaka huu.

    Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba badala ya mchezaji huyo kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizopata mfululizo.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku wa April 13, 2017 kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi.

    Simba iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kutokana na Kagera Sugar kumchezesha Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 iliyofanyika Aprili 2, 2017 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    Katika kikao chake awali Ijumaa iliyopita, Kamati baada ya kupitia malalamiko hayo, iliahirisha shauri hilo hadi leo (April 13, 2017) kujipa muda wa kufuatilia baadhi ya vielelezo kuhusu malalamiko hayo.

    “Malalamiko yaliletwa kwetu na timu ya Simba baada ya kufungwa na Kagera Sugar 2-1 kwenye uwanja wa Kaitaba, Simba walileta malalamiko kwamba kuna mchezaji mmoja wa Kagera Sugar Mohamed Fakhi alicheza mchezo huo wakati akiwa na kadi tatu za njano jambo ambalo ni kinyume na taratibu zetu kwa mujibu wa kanuni zetu za ligi,” alisema mwenyekiti wa kamati ya saa 72 wakati akitangaza uamuzi uliofikiwa na kamati yake
    .
    “Kutokana na nyaraka tulizonazo imethibitika kwamba, mchezaji huyu ambaye anaitwa Mohamed Fakhi alipata kadi ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Mbeya City, akapata kadi nyingine ya njano kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Majimaji na pia akapata kadi ya njano kwenye mchezo kati Kagera Sugar na African Lyon.”
    Kwa hali hiyo,kamati imefikia maamuzi ya kuipokonya kagera pointi na kuwapa simba na taratibu zingine zitafuata kuhusiana na hilo
    .
    Aidha amesisitiza kuwa wamechuku muda mrefu kutoa maamuzi kwa sababu ya hali ilivyokuwa, kwamba upande wa pili walikuwa wanasema rekodi zao hazioneshi hivyo kwa hiyo ilibidi tutafute rekodi za ziada ndiyo maana tumechukua muda mrefu kutoa maamuzi ya suala hili. Vinginevyo tungetoa maamuzi siku ya tarehe 7 tulipopata malalamiko haya.



    No comments:

    Post a Comment