Nyambizi
ya jeshi la Marekani imetia nanga huko pwani ya Korea Kusini huku
ikihofiwa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au
silaha za nyuklia.
Korea
Kaskazini inaadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa jeshi lake
Jumanne.na kwakuwa hivi karibuni Marekani na Korea Kaskazini wamekuwa
wakijibizana kwa kutoleana vitisho.hivyo bunge la Seneti nchini
Marekani limealikwa kwenye kikao cha kupashwa habari kuhusu Korea
Kaskazini siku ya Jumatano katika ikulu ya White House.
Nyambizi
ya USS Michigan hutumia nguvu za nyuklia na hubeba makombora aina ya
154 Tomahawk na wanajeshi 60 pamoja na meli nyambizi nyingine ndogo,
Meli hiyo inatarajiwa kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi pamoja na
kundi la meli zinazoongozwa na Carl Vinson, kundi ambalo lilitumwa
eneo la Korea kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani.
Pyongyang
ilichukizwa sana na kutumwa kwa meli hiyo na imetishia kuizamisha kwa
"shambulio moja kubwa" dhidi ya ilichosema ni uchokozi wa
Marekani.Rais wa Marekani Donald Trump alisema mapema mwezi huu
kwenye mahojiano ya runinga kwamba angetuma "kundi kubwa la meli
zenye nguvu" na kwamba Marekani ina nyambizi ambazo "zina
nguvu zaidi, nguvu zaidi kabisa kushinda meli hiyo (Carl Vinson) ya
kubeba ndege"
No comments:
Post a Comment