
Meli
kubwa ya Korea Kusini iliyokuwa na watu 24 imetoweka kusini mwa bahari ya
Atlantic.
Mabaharia
wawili raia wa Ufilipino waliokolewa, kwa mujibu wa shirika la AFP.
Siku
ya Ijumaa baharia mmoja alituma ujumbe uliosema kuwa meli hiyo yenye
urefu wa mita 312, inayojulikana kama Stellar Daisy freighter,
ilikuwa ikiingia maji.
Jeshi
la wanamaji la Uruguay lilijulisha meli nyiingine eneo hilo ambazo
zilianza kuitafuta.
Msemaji
mmoja wa jeshi naye alisema kuwa walihisi harufu kali ya mafuta,
Watu
wawili waliookolewa kwa msaada wa meli za biashara zilizokuwa
zikisaidia kutafuta meli hiyo.
Korea
Kusini pia imeomba msaada wa kuitafuta kutoka Brazil na Uruguay.
Meli
hiyo kubwa iliyo na uwezo kubeba tani 260,000 inayomilikiwa na
kampuni ya Korea Kusini, ilikuwa na raia 16 wa Ufilipinona 8 wa Korea
Kusini.
No comments:
Post a Comment