Spika
wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai leo
amemuapisha mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya
Mrisho Kikwete, Mh Salma Rashid Kikwete kuwa mbunge wa Bunge wa
kuteuliwa
Mh.Salma
kikwete aliambatana na mumewe ambaye ni rais mstaafu wa awamu ya nne Mh Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo uwepo wake ulizua shangwe na shamra
shamra miongoni wa wabunge na kuweza kuonesha hisia zao waziwazi za
kumkumbuka kwa uongozi wake uliomalizika.
Leo
hii Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limeanza kikao chake cha
kwanza cha mkutano wa bajeti
Mama
Salma Kikwete kama anavyotambulika na walio wengi nchini ni mjumbe wa
halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi taifa{CCM}, lakini pia
inatajwa kuwa ni miongoni mwa wanawake wenye ushawishi mkubwa kweye
jamii,thamani ya mwanamke ilindwe kwa maslahi ya taifa.
No comments:
Post a Comment