Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) nchini Tanzania imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoaanza kutumika kuanzia leo.
Akitangaza
bei hizo leo Meneja wa Mawasiliano wa Ewura Tanzania ,bwana Titus
Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 na itauzwa
kwa Sh 2057 kutoka 2060, huku dizeli ikipanda kwa Sh 12, kutoka Sh
1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka1952
Bwana Titus Kaguo ameeleza kuwa "Mabadiliko haya kwenye bei kwa mafuta ya petroli na Dizeli yametokana na bei za mafuta hayo kubadilika kweye soko la dunia pamoja na mfumuko unaobeba gharama za usafirishaji ikilinganishwa na hapo kabla".
No comments:
Post a Comment