Taarifa za toka kwenye vyombo vya usalama nchini Nigeria, imeeleza kufichuliwa zaidi ya dola milioni 40, iliyo kwenye sarafu ya pesa za Nigeria na ya kimataifa, baada ya msako wa ghafla kwenye nyumba moja mjini Lagos.
Tume ya kupambana na uhalifu wa uchumi na kifedha (EFCC), imesema kuwa, ilipata “noti nyingi za Marekani, pouni ya Uingereza na nyingine za naira, kwenye mifuko iliyokuwa imefungwa barabara, ndani ya nyumba moja yenye vyumba vinne vya kulala.
Inasema
kwamba wapelelezi waliingia kwa nguvu ndani ya nyumba hiyo na kunasa
dola milioni 43 nukta 4, Pauni Milioni 27 na laki 8 na Naira milioni
23 nukta 2, taslimu.
Aida
taarifa zinasema kuwa, baada ya kupekuwa zaidi mojawepo nya vyumba
hivyo, walipata pesa zaidi ndani ya kabati la nguo,inasemekana kuwa
fedha hizo zinaaminika kupatikana kupitia njia haramu.
Tume
ya EFCC, inasema kuwa, mfichuzi wa kashfa hiyo, aliwajulisha
wapelelezi kuhusiana na mienendo iliyojaa shaka kuhusiana na mabegi
yaliyokuwa yakiletwa na kutolewa kwenye nyumba hiyo mara kwa mara.
Maelezo
toka kwa mmoja wa majirani wa karibu na nyumba hiyo, amefichua kuwa,
“Mwanamke
mmoja amekuwa akionekana katika jumba hili mara kwa mara akiwa na
mabegi yenye maandishi Ghana Must Go. Alikuwa akionekana mwenye
uchovu, mavazi machafu na mwenye wasiwasi mwingi, lakini urembo wake
haukuwa ukiendana na mavazi hayo, pengine kujifanya ili
asitambuliwe.” alisema jirani huyo.
Taarifa
nyingine zinasema kuwa, maafisa wa usalama waliwahoji walinzi katika
eneo hilo na wakasema kuwa hakuna mtu aliyekuwa akiishi katika jumba
hilo.
No comments:
Post a Comment