Staa
wa Bongofleva kutoka kundi la Weusi ambalo limekuwa linafanya vizuri
kunako anga za muziki wa bongo na Afrika,Bonta leo 13/04/ 2017
kupitia kipindi cha XXL ya Clouds amezungumzia juu ya kutoonekana
mara kwa mara kwenye shughuli za kundi.
Bonta haonekani kwenye kundi la WEUSI kama wafanyavyo Nikki wa Pili, Joh makini na Gnako na hajasita kulisemea hilo akisema amekuwa mbali kutokana na majukumu ambayo yanamfaya awe mbali kwenye baadhi ya kazi zinazofanywa na wana kundi.
Bonta ambaye ndiyo CEO wa kampuni ya WEUSI ambayo imesajiliwa kibiashara amesema ”Weusi siyo kama bendi ya Dansi. Nipo mbali nao kimajukumu,ndio maana nakosekana kwenye kazi nyingi. Mimi ndiyo CEO wa WEUSI Kampuni tumeweza kuisajili kibiashara kabisa na tunaweza tusiwe marafiki kwenye muziki ila ni marafiki kifamilia. Mimi na Joh Makini tumetoka mbali pamoja na Lord Eyez.” Bonta.
Alipoulizwa kuhusu wimbo wake mpya alioutambulisha leo kupitia kipindi hicho, Bonta alisema “Ngoma yangu mpya inaitwa Ziro inazungumzia juu ya mfumo mzima wa Elimu; kuanzia elimu ya msingi hadi Chuo na nimerekodi tangu mwaka jana. Sijazungumzia kuhusu mtu mmoja, imezungumzia mfumo na huu ndiyo wakati wake.”Bonta.

No comments:
Post a Comment