TFF kamati ya katiba na hadhi za
wachezaji yawarudishia kagera sugar pointi zao za mchezo walioshinda dhidi ya wekundu wa msimbazi "Simba SC",katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema kuwa matokeo yaliyotokea siku ya mchezo wa timu hizo mbili yatabaki
kama yalivyokuwa awali.hivyo hii ina maana kuwa malalamiko
yaliyotolewa na simba na maamuzi yaliyochukuliwa yametupiliwa mbali
baada ya kamati kukaa na kupitia kanuni zinazowaongoza kiutendaji.
“Kikao cha kamati ya masaa 72
kimeonekana kukosa uhalali,kwa kuwashirikisha wajumbe walioonekana
kutokuwa sehemu ya kamati hiyo”.
“Walioonekana kupotosha kamati bodi
ya ligi itashughulika nao baada ya kupata majina yao,hivyo hata
nafasi za msimamo wa ligi utaonekana katika mtazamo mpya sasa”.
No comments:
Post a Comment