The blues Chelsea imefanikiwa kutinga
hatua ya fainali kwenye kombe la FA baada ya kuwabamiza Totenham
hotspurs mabao 4-2 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye
uwanja Wembley.
Chelsea ilipata bao la kwanza kupitia
kwa mchezaji Willian katika dakika ya 5 ya mchezo kwa mpira wa adhabu
ndogo na kwenda moja kwa moja wavuni,baada ya dakika kumi kupita pale
mshambuliaji wa spurs Harry kane alipo ilisawazishia spurs kwa mpira wa
kichwa baada ya kupokea pande zuri kutoka upande wa kulia,kwa mara
nyingine Willian akaiandikia Chelsea bao lingine dakika ya 43 kwa
mkwaju wa penalti wakati bao lingine la Chelsea limefungwa na Nemanja
Matic dakika ya 80 goli la pili la spurs lilifungwa na Dele Alli
dakika ya 52.
Kwa matokeo hayo sasa Chelsea itakutana
na mshindi kati ya Arsenal na
Manchester City zitakazokutana hapo
kesho kwenye uwanja wa Wembley.
No comments:
Post a Comment